ANNA PETER

Music when healthy, is the teacher of perfect order

WE COVER EVERY NETWORK

When words leave off, music begins.

MISTARI

The wise musicians are those who play what they can master.

ENTERTAINMENT

Who hears music feels his solitude peopled at once.

Welcome to anapita.com

Where music lives

Tuesday, August 16, 2016

Sina tatizo la Baraka Da Prince- Young Killer

Rapa Young Killer anayeiwakilisha Mwanza katika muziki wa Hip hop amefunguka na kusema kuwa yeye hana tatizo lolote na msanii mwenzake Baraka Da Prince ambaye anatokea Mwanza pia na kusema yeye ni shabiki wa msanii huyo kwa sababu anafanya kazi nzuri.

Young Killer anasema kwamba hata yeye kuna maneno aliyasikia lakini anaamini yeye hana tofauti yoyote na msanii huyo anamkubali kutokana na kazi yake nzuri anayofanya kwenye muziki wa bongo fleva.

Mbali na hilo Young Killer amesema kuwa kwa sasa ataendelea na utaratibu wake wa kutoa wimbo kila baada ya miezi mitatu na anafanya hivyo kutokana na ukweli kwamba wasanii wengi wanakuwa wanatoa ngoma hivyo anaona akikaa kimya itamfanya apotee kwenye game.

Hata ukisema nije kuimbia kuku ambao hawatagi nakuja- Peter Msechu

Msanii Peter Msechu ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wa 'Mama' ambao ni wimbo wa kushirikiana kati yake na Banana Zoro, Msechu amesema kuwa yeye pamoja na Banana Zoro hawachagui show hata ukitaka kuwaita waje kuimbia kuku wako ambo hawatagi ili watage wao watakuja cha msingi wao wanaingiza pesa.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet bongo Peter Msechu alisema kuwa amejifunza kuwa katika maisha ya kila siku ukifanya jambo lako na kumgusa mwanamke au mama hilo jambo lazima litafanikiwa.

"Yanii sisi saizi hata ukija ukiniambia Msechu tunahitaji Band yako ije iimbie kuku wetu ambao hawatagi ili watage sisi tunakuja tunafanya yetu, maana kama daktari amekwambia hao kuku hawatagi mpka waimbiwe sisi tunaimba tu" alisema Peter Msechu

Inde ndiyo Pogba na mimi ni chatu- Dully Skyes

Msanii Dully Skyes amefunguka na kusema kuwa kwa sasa yeye anafahamika kama Chatu na kazi yake ni kuwanyonga

Dully Skyes akiongea na Anna peter anasema kuwa kwa sasa kwa kuwa mchezaji mpira wa Manchester United ndiyo habari ya mjini na wimbo wake mpya yeye 'Inde' ni habari ya mjini basi wimbo huo ni sawa na Pogba na yeye saizi anafahamika kama CHATU kwani anawanyonga.


Mbali na hilo msanii Dully Skyes anasema kuwa mashabiki wamekuwa wakimfananisha na Kanye West katika uvaaji ndiyo maana hata yeye saizi amekuwa akipenda kuvaa kama msanii huyo kutoka Marekani kwani anamkubali na anavutiwa naye.

Monday, August 15, 2016

Machozi ya mwanamke huwa na laana- Ben Pol

Msanii Bel Pol amewapa fundo baadhi ya wanaume ambao wamekuwa wakiwaumiza na kuwatesa wapenzi wao wa kike kiasi cha kuwaliza kila siku na kuwafanya wajutie maisha yao, Ben Pol anasema kumliza mwanamke asiye na hatia ni laana ambayo mwisho wa siku itakuja kukusumbua.

Ben Pol ametumia mtandao wake wa Instgram kuandika ujumbe huo na kuwakumbusha kutowatumia wanawake kwa maslahi yao binafsi na kuja kuwaacha kwani kufanya hivyo ni kuwatengenezea maumivu na mateso.

'Machozi ya mwanamke asiye na hatia huwa na laana kubwa kuliko unavyofikiria, usimpe nafasi mwanamke akatoa chozi na kumlilia Mungu kwa mateso na unyanyasaji unaomfanyia, usipompenda, mwache kwa wema.. Usimtumie kwa maslahi yako binafsi na baadaye ukamtupa. Uchungu unaoupata unapomwona mama yako anasumbuliwa na baba yako ndiyo uchungu wanaoupata wanawake wote wema unaowatesa" aliandika Ben Pol

Wimbo wa Nay wa Mitego 'Pale kati patamu' bado ni tatizo- BASATA

BASATA wamesema licha ya msanii Nay wa Mitego kufanya marekebisho mara mbili kwenye wimbo wake 'Pale Kati patamu' uliofungiwa na BASATA kutokana na kuto kuwa na maadili bado wimbo huo haustahili kuendelea kuchezwa kwenye vyombo vya habari.

"Tumemfungulia Msanii Nay wa Mitego kwa kutekeleza maagizo aliyopewa, kujutia na kukiri kubadilika. Wimbo wa 'Pale Kati' bado haukidhi. Pamoja na kuufanyia marekebisho mara mbili wimbo wa Pale Kati bado haukidhi. Tunaendelea kuufungia hadi itakapoelekezwa vinginevyo, tunatoa maelekezo kwa vyombo vya habari kutocheza wimbo wa 'Pale Kati'. Hatua na adhabu za kisheria zitachukuliwa kwa atakayekaidi" wamesema BASATA

Friday, August 12, 2016

Kitu ambacho Jux akipendi kwenye mwili wake

Msanii Juma Jux amesema kuwa katika vitu ambavyo havipendi kwenye mwili wake basi ni miguu yake, anasema kutokana na hilo inafikia hatua akivaa kaptula anaamua kuvaa na soksi kwa sababu hapendi kuiona miguu yake hiyo.

Jux anasema mara nyingi hapendi kuvaa kaptula kwani anapozivaa inakuwa rahisi kwake kuiona miguu yake hiyo ambayo yeye haipendi, ila anadai siku akijisikia kuvaa kaptula lazima avae soksi tena ndefu ili tu asione miguu hiyo


Ridhiwani Kikwete awapongeza Alikiba na Diamond Platnumz

Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhani Kikwete amewapongeza wasanii wa bongo fleva Alikiba pamoja na Diamond Platnumz kwa moyo wao wa kujitolea na kusaidia katika jamii baada ya wasanii hao kila mmoja kwa nafasi yake kuweza kuchangia pesa kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaofanyia upasuaji wa vichwa vikubwa.

Ridhiwani Kikwete alitumia mitandao yake ya kijamii kuwapongeza wasanii hao kwa kuguswa na kuisaidia jamii na kusema huo ni mfano na kitendo hicho kimeonyesha umuhimu wa kuwa na watu maarufu kwenye jamii

"Katika vitu vimeonyesha umuhimi wa kuwa Star katika jamii yetu ni hili mlilolifanya wadogo zangu. Ni jambo la kusifiwa na mungu atawalipa kwa kuwaongezea maarifa ya kufanya kazi zenu vizuri. Pia niwapongeze sana @gsmfoundationtz @gsm_foundation kwa kazi nzuri mnayoifanya. Kutoa si utajiri, ni moyo na mungu atakuzidishia ndg mkurugenzi Gharib pale ulipotoa. Kila la kheri katika kusaidia jamii yetu yenye mahitaji. Peace to you"- Ridhiwani Kikwete

VIDEO DULLY SYKES FT HARMONIZE - INDE

Thursday, August 11, 2016

Collabo zimenibeba sana- Chin Beez

Msanii Chin Beez amefunguna na kusema kuwa collabo alizofanya siku za karibuni zimeweza kumfikisha mahali fulani pazuri ambapo tayari watanzania wameanza kumtambua na kuona uwezo wake katika uimbaji.

Chin Beez alisema kuwa kupitia collabo hizo kadhaa watu wameweza kuona ukali wake, Chin Beez mpka sasa amefanya collabo kubwa tatu ambazo zinafanya vizuri sasa ikiwepo 'Arosto' ya G Nako, amefanya collabo na Quick Racka kwenye wimbo wa 'Mwendo kasi' lakini pia amefanya collabo na Niki wa Pili kwenye wimbo wake mpya 'Sweet Mange'

Diamond Platnumz atangaza neema

Msanii Diamond Platnumz ametangaza neema kwa vijana ambao wanaweza kuungana na kucheza wimbo wake wa Kidogo ambao ameshirikiana na P Square na kusema kikundi ambacho kitakuwa kimechezwa haswa kitapewa pesa taslimu milioni tano.

Katia ujumbe wake huo Diamond amesisitiza kuwa vijana hao wanatakiwa kuchanga na style zao wenyewe ili tu wanatakiwa kuwa wameua kweli si kitoto ili kushinda pesa hizo


"NIKO na MILIONI 5 Cash Mkononi kwa kikundi kitachotuma clip ya kudance #KIDOGO sawia haswaaaa!!! yani sio kiwasiwasi waue Haswaaaa....... tena wamix na style zao wenyewe... Narudia tena Wauwe haswaaa!!!... haya wapigie simu wanao Mjipange kesho Mtume clip kwa namba hii +255654019091 na mkisha tuma mpandishe insta na kuhashtag neno #KIDOGO .... na kesho hiyo ntatangaza Mshindi Anapatikanaje"